• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanakijiji aanzisha kampuni ya chai kusaidia kuondoa umaskini

  (GMT+08:00) 2017-07-19 19:15:59

  China ni chimbuko la chai. Mkoa wa Guizhou nchini China una maeneo makubwa zaidi yanayolimwa chai. Lakini kaunti ya Songyan ya mkoa huo, ni eneo maskini zaidi nchini kote. Wanakijiji wengi wa kaunti hiyo wanakwenda nje kutafuta kazi. Lakini, baada ya jitihada zilizotofanywa na serikali na watu wa pale, kaunti hiyo imeanza kuondoa umaskini. Mwenyeji wa huko aliyewahi kufanya kazi nje, Bw. Luo Digang amerudi nyumbani kwao na kuwa mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya chai wa huko.

  Kabla ya kuanza mahojiano na Bw. Luo, aliwaalika waandishi wa habari kunywa chai ya Ganjing ambayo ni bidhaa maarufu ya kampuni yake ya chai ya Fengxiangyuan. Alisema chai hiyo imekidhi vigezo vya Ulaya katika kutokuwa na dawa za kuua wadudu na uchafuzi wa metali nzito. Hivi sasa, chai hiyo inauzwa si nchini China tu, bali pia inauzwa barani Ulaya na Afrika.

  Bw. Luo amesema ingawa aliweza kuchuma pesa nje ya kijiji chake, lakini, hakuweza kuwatunza vizuri watoto na wazazi wao. Kutokana na kuhamasishwa na serikali, aliamua kurudi nyumbani kuanzisha biashara.

  Mwenzake Bw. Xu Xing ambaye ni meneja mkuu wa kampuni hiyo, amesema, mwanzoni walihimiza wakulima 200 kupanda chai na kununua majani ya chai hizo kwa bei ya kawaida ya sokoni. Ingawa jambo hilo linaonekana rahisi, lakini walikabiliana na matatizo mengi, ikiwemo kuwashawishi wakulima kukodisha mashamba yao.

  Bw. Xu amesema, katika miaka 7 iliyopita, waliendelea kuwekeza kwenye kampuni hiyo, lakini kampuni hiyo inatarajia kupata faida kuanzia mwaka kesho. Wenyeji wengi wa kaunti hiyo wameacha nyumba zao za kale na kujenga nyumba mpya kutokana na mapato mazuri ya kupanda chai.

  Akiuliza ni kwa nini ameendeleza chapa hiyo ya chai inayohitaji uwekezaji mkubwa, Bw. Xu amesema, ubora ni muhimu. Familia yake yote wanakunywa chai hiyo ya Ganjing. Amesema, ingawa bei ya chai hiyo ni ya juu kidogo, lakini ni sahihi kujitahidi kuhakikisha ubora na usafi wa chai.

  Katibu wa chama wa kaunti hiyo, Bw. Li Yi amejulisha kuwa, hivi sasa pato la wastani la mwaka la kaunti hiyo kwa kila mtu limefikia yuan 8,960. Katika siku za baadaye, kaunti hiyo inaweza kuondoa umaskini na kuwa kaunti tajiri, yenye mandhari nzuri na maendeleo zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako