• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Wang Yi aeleza msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ghuba

    (GMT+08:00) 2017-07-20 09:58:55

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alikutana na waziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa falme za Kiarabu Sultan al Jaber ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Wang Yi amesema China ikiwa ni rafiki wa nchi za Ghuba, inatumai na kuamini kuwa nchi hizo zinaweza kutatua mgogoro huo kwa njia mwafaka.

    Amesema, China inataka suala hilo litatuliwe kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia ndani ya mfumo wa Kamati ya ushirikiano wa nchi za Ghuba, na pia inatoa wito kwa pande husika kuanza mazungumzo kwenye msingi wa kukubaliana kupinga ugaidi wa aina yote.

    Amesema China inaamini pande husika ikiwemo Umoja wa Falme za Kiarabu zina uwezo wa kudhibiti hali ya sasa, na kutatua mgogoro kwa njia yenye busara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako