• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda Akaunti ya sasa ya serikali ya Uganda fedha zake zimepungua na dola milioni 43.9

    (GMT+08:00) 2017-07-20 19:52:02
    Akaunti ya sasa ya serikali ya Uganda fedha zake zimepungua na dola milioni 43.9 hadi dola milioni 131 katik robo iliyomalizika mwezi Aprili 2017.

    Kushuku huku kumetokana na kushuka kwa uagizaji wa serikali na pia kushuka kwa mahitaji ya watumiaji wa ndani.

    Takwimu za hivi karibuni kutoka Benki ya Uganda (BoU) zinaonyesha kuwa uagizaji wa jumla ulipungua kwa asilimia 2.2 kati ya mwezi Februari na mwezi Aprili mwaka 2017 sawa na dola milioni 24 sana sana kutokana na uingizaji vifaa vya miradi ya Serikali.

    Mapato ya mauzo ya nje pia yalishuka kwa asilimia 5.8 wakati huo huo.

    Upungufu mdogo unamaanisha shinikizo la chini kwa Shilingi ya mashirika ya serikali na wafanyabiashara wa ndani wanaotaka kununua dola ili kulipia uagizaji.

    Mnamo mwezi Aprili 2017, kiwango halisi cha ubadilishaji kilipungua kwa asilimia nne ikilinganishwa na kushuka kwa thamani ya asilimia 3.9 mwezi Machi 2017.

    Kiwango cha mfumuko wa bei kilifika asilimia 5.7 mwezi Februari lakini kilishuka hadi asilimia 4.7 mwezi Machi, kabla ya kupanda kwa asilimia 4.9 mwezi Aprili 2017, takwimu za BoU zinaonyesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako