• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars kuchuana na Amavubi kuamua mshindi

    (GMT+08:00) 2017-07-21 11:23:31

    Makocha wa timu za soka za Tanzania na Rwanda wameelezea Imani yao kuwa vikosi vyao vitafanya vyema katika mchuano wa kufa kupona baina ya timu hizo hapo kesho.

    Kocha wa Taifa Stars Salum Maganga anasema wachezaji wake wako katika hali chanya kiakili huku akidumisha kuwa timu yake itafuzu mashindano ya CHAN itakayoandaliwa mwakani.

    Kwa upande wake, mkufunzi wa Amavubi Stars Antoine Hey anashikilia msimamo kuwa kucheza nyumbani kutawapa wachezaji wake motisha zaidi kushinda timu ya Tanzania katika mechi hii ya marudiano.

    Mechi hii itasimamiwa na marefa kutoka Uganda. Timu hizo zilitoka sare bao 1-1 wikendi iliyopita. Mshindi atachuana na Uganda au Sudan Kusini kabla ya kukata tiketi ya CHAN.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako