• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Afghanistan limewaua waasi 98 ndani ya siku moja

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:38:34

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema vikosi vya usalama nchini humo vimewaua waasi 98 kote nchini kuanzia mapema jana.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya nchi hiyo inasema, ndani ya muda wa saa 24 vikosi hivyo vilifanya operesheni ya kupambana na ugaidi na maadui wa amani na utulivu, na kufanikiwa kuwaua waasi 98 na kuwajeruhi wengine 36. Taarifa imesema kati ya waliouawa kuna wafuasi kadhaa wa kundi la Taliban na wafuasi wanne wa kundi la IS.

    Vikosi hivyo pia vilifanikiwa kukamata baadhi ya silaha nyepesi na nzito, kwenye majimbo 13 kati ya majimbo 34 ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako