• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa YouthConnekt Afrika wafunguliwa nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:42:18

    Mkutano wa YouthConnekt Afrika ulifunguliwa jana huko Kigali nchini Rwanda. Washiriki wa mkutano huo wanaona ujasiriamali na uvumbuzi wa vijana utahimiza utatuzi wa tatizo la ukosefu wa ajira. Kwenye mkutano huo wajumbe zaidi ya 2800 kutoka nchi 90 wanajadili kuhimiza uwezo wa vijana barani Afrika.

    Mkurugenzi wa benki ya maendeleo ya Afrika Bw. Akinwumi Adesina amesema, mustakabali wa vijana barani Afrika uko barani Afrika, si Ulaya au chini ya Bahari ya Mediterranean. Amesema vijana wa Afrika wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwa kuwa wavumbuzi na wajasiriamali. Vilevile amesema benki ya maendeleo ya Afrika itaunga mkono wavumbuzi na wajasiriamali vijana kupitia uchangishaji wa fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako