• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono kuendelea kutekeleza makubaliano ya suala la nyuklia la Iran kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2017-07-22 17:18:34

    Nchi sita za suala la nyuklia la Iran zikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China na Ujerumani na Iran jana mjini Vienna Australia zilifanya mkutano wa nane wa tume ya ushirikiano ya makubaliano ya suala la nyuklia la Iran. Katibu mkuu wa idara ya shughuli za nchi za nje za Umoja wa Ulaya Bw. Helga Schmid ameendesha mkutano huo, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bw. Tom Shannon, naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Abbas Araqchi na maofisa husika wa Russia, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani walihudhuria mkutano huo. Mkuu wa idara ya udhibiti wa jeshi ya wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Qun aliongoza ujumbe wa China kuhudhuria mkutano huo.

    Bw. Wang Qun amesema kuwa China itaendelea kuunga mkono na kulinda makubaliano ya pande zote. Amesisitiza umuhimu wa makubaliano ya pande zote, akisema kuwa pande zote zinapaswa kuimarisha maoni ya siasa, kutekeleza jukumu kwa dhati, kutatua mgogoro kwa njia muafaka ili kuhakikisha makubaliano hayo yatekelezwe kwa pande zote na halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako