• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jordan Spieth amkabili vilivyo Matt Kuchar na kushinda The Open

  (GMT+08:00) 2017-07-24 10:59:20

  Jordan Spieth alishinda mashindano ya The Open katika uwanja wa Royal Birkdale kwa shoti tatu baada ya mechi ya kukata na shoka baina yake na Matt Kuchar.

  Spieth, mwenye umri wa miaka 23, aliachilia uongozi wake wa shoti tatu na kujipata akiwa nyuma ya Kuchar baada ya kushindwa shoti kwenye hawamu ya 13.

  Lakini alitia ushindani mkubwa na kurejesha uongozi wake na kushinda msururu wa birdie, eagle, birdie na birdie nyingine na kuhakikisha ushindi wa taji lake kuu la tatu baada ya the Masters na US Open.

  Mwamerika huyo ni mchezaji wa pili baada ya Jack Nicklaus kushinda mataji matatu ya gofu baina ya mataji kuu nne kabla ya kuitimu miaka 24. Aidha, Spieth ni mchezaji mwenye umri mdogo tangu Seve Ballesteros aliyekuwa na umri wa miaka 22 aliposhinda mataji matatu mwaka 1979

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako