• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya na Nigeria zatakiwa kujiunga na makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa mafuta ghafi

    (GMT+08:00) 2017-07-24 19:25:59

    Waziri wa nishati wa Russia Bw. Alexander Novak amesema, Libya na Nigeria ambazo zimepata msamaha wa kupunguza mafuta kutoka shirika la nchi zinazozalisha mafuta OPEC, zinatakiwa kujiunga na makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa mafuta ghafi baada ya uzalishaji wa nchi hizo mbili kuwa imara.

    Bw. Novak amesema, utulivu wa uzalishaji wa mafuta ghafi utasaidia kupunguza mabadiliko ya soko la mafuta ghafi la kimataifa. Amesema, mkutano wa kamati ya usimamizi wa ngazi ya mawaziri wa nchi zinazozalisha mafuta za OPEC na zisizo za OPEC unaofanyika huko St. Petersburg nchini Russia utajadili suala la uzalishaji wa mafuta la nchi hizo mbili.

    Mwishoni mwa mwaka 2016, Shirika la OPEC na nchi nyingine 11 zisizo za shirika hilo ikiwemo Russia zilifikia makubaliano ya kupunguza uzalishaji. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu, nchi hizo zinapaswa kupunguza uzalishaji wa mapipa milioni 1.8 kwa siku. Libya na Nigeria zimepata msamaha wa kupunguza uzalishaji kutokana na hali ya vurugu za ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako