• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yakanusha kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-07-25 10:03:52

    Serikali ya Tanzania imesisitiza tena kwamba haiingilii kati uchaguzi mkuu wa Kenya.

    Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga amesema ripoti husika zilizotolewa na vyombo vya habari vya Kenya kuhusu Tanzania kuingilia uchuguzi mkuu wa Kenya hazina msingi. Amesema kamwe Tanzania haitaingilia mambo ya ndani ya nchi za nje, ikiwemo uchaguzi mkuu wa Kenya.

    Baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti kwamba kiongozi wa chama cha upinzani cha Kenya Raila Odinga ameweka kituo cha kuhesabu kura nchini Tanzania ili kuhakikisha hakuna hila kwenye upigaji kura.

    Bw Mahiga ameongeza kwamba Tanzania inathamini sana uhusiano kati yake na Kenya uliodumu kwa miaka mingi, na kamwe haitaingilia kati mambo ya ndani ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako