• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jordan yatoa mwito kwa Israel kuchukua hatua kurejesha utulivu eneo la Temple Mount

    (GMT+08:00) 2017-07-25 10:21:46

    Mfalme Abdullah II wa Jordan amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Bw Benjamin Netanyahu kwa njia ya simu na kutoa mwito kwa Israel kuchukua hatua za kutuliza hali ya eneo la Temple Mount mjini Jerusalem.

    Mfalme Abdullah amesisitiza kuwa Israel inapaswa kuondoa vizuizi dhidi ya eneo hilo ili kusimamisha makabiliano mapya kati ya Israel na Palestina. Pia amesema ni bora Israel ifikie makubaliano na Jordan katika kuzuia hali ya sasa, na kuheshimu hadhi ya kihistoria na hali halisi ya msikiti wa Al-Aqsa.

    Habari nyingine zinasema wafanyakazi wa ubalozi wa Israel nchini Jordan akiwemo mlinzi mmoja aliyewapiga risasi wajordan wawili baada ya kuchomwa kisu nje ya ubalozi huo, wamerudi Israel jana usiku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako