• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wakulima wahimizwa kutumia mawazo ya kilimo biashara kuboresha mazao yao

    (GMT+08:00) 2017-07-25 19:16:50

    Wakulima nchini Kenya wamehimizwa kutumia mawazo kutoka maonyesho ya kilimo kubadilisha teknolojia za kilimo na kuboresha kilimo katika kanda.

    Akizungumza wikendi iliyopita wakati wa maonyesho ya kilimo biashara katika taasisi ya sayansi na teknolojia ya Rift Valley Institute of Science and Technology, Afisa mkuu wa kilimo Stanley Chepkwony aliwaambia wakulima kwamba mawazo kutoka kwa wataalamu wakati wa sherehe kama hizo yanasaidia sana kufufua kilimo.

    Alisema mikutano kama hiyo husaidia wakulima kupata ujuzi kuhusu njia bora za kilimo,aina mpya za mimea,wanyama na njia nzuri za usimamizi ambazo zinaweza kuboresha kilimo chao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako