• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Kichinjio cha punda cha Naivasha chafunguliwa tena baada ya kufanyiwa ukarabati

    (GMT+08:00) 2017-07-25 19:17:10

    Kichinjio cha punda cha mjini Naivasha,nchini Kenya,kimefunguliwa tena baada ya kufungwa na idara ya mifugo miezi miwili iliyopita.

    Kichinjio cha Star Brilliant kilichoko eneo la Kinamba mjini Naivasha kilifunguliwa upya juzi baada ya kufanyiwa ukarabati.

    Kichinjio hiki kilifungwa miezi miwili iliyopita baada ya uchunguzi uliofanywa na shirika la ulinzi wa wanyama na idara ya mifugo kubaini kuwa kichinjio hicho kilivunja sheria kwa kuchinja na kuwachuna ngozi punda ilhali wengine walio hai wakiwa wanaona.

    Akithibitisha kufunguliwa upya kwa kichinjio hicho,mkurugenzi wa huduma za mifugo katika kaunti ya Nakuru Dkt Enos Amuyunzu alisema kichinjio hicho kimepewa ruhusa ya kufungua tena baada ya ukarabati na kufuata sheria.

    Alisema kuwa maafisa walizuru kichinjio hicho na kuthibitisha kuwa kimetekeleza na kuafiki viwango vinavyohitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako