• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa vyombo vya habari vya kisasa vya mtandao kati ya China na Tanzania wafanyika Dar es Salaam

  (GMT+08:00) 2017-07-26 10:18:43

  Mkutano wa vyombo vya habari vya kisasa vya mtandao wa Internet kati ya China na Tanzania, umefanyika jana mjini Dar es Salaam, Tanzania.

  Naibu mkurugenzi wa ofisi ya habari ya mtandao wa taifa ya China Bw. Ren Xianliang amesema, vyombo vya habari ni daraja muhimu la kuhimiza maelewano kati ya nchi hizo mbili. Amependekeza kuongeza ushirikiano wa kutangaza urafiki kati yao, na kupanua ushirikiano wa vyombo vya habari vya kisasa kati yao ili kusukuma mbele mawasiliano ya vyombo vya habari vya kisasa.

  Naibu waziri wa ujenzi, usafiri na mawasiliano wa Tanzania Bw. Edwin Ngonyani amesema, teknolojia ya mtandao wa internet imechukua nafasi muhimu katika kuhimiza maendeleo ya vyombo vya habari. Katika miaka za hivi karibuni, maendeleo ya teknolojia yamebadili hali ya vyombo vya habari, na kuleta changamoto mpya ya kulinda usalama wa mtandao wa internet.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako