• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya kuendesha baiskeli ya Rwanda yapanda ngazi

  (GMT+08:00) 2017-07-26 10:40:08

  Rwanda imeinuka kutoka nafasi ya sita hadi nne kwenye jedwali iliyotolewa karibuni la umoja wa waendeshaji baiskeli duniani UCI. Ni mafanikio ya kihistoria kwa kikosi cha wanabaiskeli cha wanaume ya Rwanda baada ya miaka nyingi ya kutia bidii.

  Baada ya taarifa hiyo kutolewa, mwenyekiti wa shirikisho la wanabaiskeli ya Rwanda Aimable Bayingana alisema kuinuka kwa viwango vya timu hiyo inatoa motisha ya kufanya vyema zaidi siku za baadaye.

  Bayingana alisema wanafurahi kuwa nambari nne barani Afrika, na kusema kuwa lengo sasa ni kusonga mbele na wala si kurudi nyuma. Hata hivyo anasema hii inachangamoto zake kwani timu hiyo sasa lazima ishiriki mashindano mengi ya kimataifa na kutafuta ushindi.

  Timu ya Eritrea ilirejea kileleni na kuwa namba moja, mbele ya Morocco ilhali Afrika Kusini inakamilisha jedwali la tatu bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako