• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TRA yafunga maduka ya wafanyabishara wasiotumia mashine za kielektroniki

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:30:26

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefunga maduka ya wafanyabishara wasiotumia mashine za kielektroniki za EFD.

    Hatua hiyo imekuja baada ya maofisa wa TRA kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa na kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaodaiwa kutokuwa na mashine za kutolea risiti za EFD.

    Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Lampson Tulianje amesema wafanyabishara hao wamekaidi agizo la Serikali la kutakiwa kuwa na mashine kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

    Tulinje amefafanuaa kuwa lengo la kufikia hatua hiyo ni kuhimiza wafanyabiashara hao kulipa kodi stahiki kwa kutumia mashine hizo ambazo zina uwezo wa kuweka kumbukumbu vizuri za mauzo ya bidhaa zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako