• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunda mfumo wa bei za bidhaa unaoamuliwa na soko

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:35:19

    Kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa ya China imesema, katika miaka ya hivi karibuni mageuzi ya bei za bidhaa yamepiga hatua kubwa nchini China, mfumo wa bei kuamuliwa na soko umeundwa kwa kiasi kikubwa, ambapo bei ya mazao yote ya kilimo imeamuliwa na soko.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya bei ya kamati hiyo Bw. Peng Shaozong amesema, mwaka 2016 kiwango cha bei zilizosimamiwa na serikali ya China kilikuwa chini ya asilimia 3 ambayo imepungua kwa asilimia 2.68 kuliko mwaka 2012. Kufuatia kufunguliwa sekta ya gharama ya kununua tumbaku katika mwaka 2015 , bei za mazao yote ya kilimo zimeamuliwa na soko.

    Bw. Peng pia amesema, kiwango cha bei za bidhaa zinazosimamiwa na serikali kuu kimepungua kwa kiasi kikubwa, mageuzi ya bei katika sekta muhimu yanaendelea kusukumwa mbele, ambayo yanainua kiwango cha bei kuamuliwa na soko kwa kiasi kikubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako