• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rayon Sports kushiriki sherehe za Simba Day

    (GMT+08:00) 2017-07-27 10:31:19
    Klabu ya Simba ambayo ni mjumbe wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la CAF, Iimealika mabingwa wa Rwanda, Rayon Sports kushiriki sherehe ya kila mwaka ya klabu hiyo maarufu 'Simba Day' kabla ya kuanza kwake Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Kwenye taarifa kutoka kwa wasimamizi wa klabu hiyo, Simba imealika mabingwa hao wa ligi kuu ya Rwanda kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, ambazo kwa kawaida hutumika kutambulisha kikosi kipya cha klabu hiyo kwa mashabiki.

    Rayon itachuana na Simba katika mechi itakayotumika kutambulisha sare mpya ya msimu unaofuata. Kila mwaka Simba Day inasherehekewa kwa minajili ya kuwaleta karibu klabu na wafuasi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako