• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la majini la China latekeleza majukumu mengi zaidi ya kimataifa na kupiga hatua kufikia kiwango cha juu duniani

  (GMT+08:00) 2017-07-27 18:11:43

  China ni nchi yenye eneo kubwa la bahari ambayo ina ufukwe wenye urefu wa kilomita elfu 18, na eneo la bahari lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba milioni 3. Jeshi la majini la China linasifiwa na meli za biashara za nchi mbalimbali zinazopita katika Ghuba ya Aden kuwa ni "mwavuli wa ulinzi" unaoaminika, na pia linafurahiwa na wanamaji wa nchi nyingine duniani. Je, ni vipi jinsi ya jeshi la majini la China linatekeleza majukumu mengi zaidi ya kimataifa, na kuwa na uwezo mkubwa wa kufikia kiwango cha juu duniani?

  Kikosi cha timu ya nyambizi kwenye Bahari ya Mashariki ya jeshi la majini la China kinatekeleza jukumu kwenye eneo lililoko umbali mkubwa kutoka China. Hivi sasa jukumu kama hilo linatekelezwa mara kwa mara na kuwa kazi ya kawaida kwa timu ya nyambizi za China. Nahodha wa nyambaizi hiyo Yu Ping amemwambia mwandishi wa habari kuwa, kutokana na kuwepo kwenye sehemu maalumu, kikosi hicho kinakabiliana na majukumu mbalimbali, na kiwango cha kufanya mazoezi pia kinazidi kuimarishwa. Anasemaļ¼š

  "Hapo awali, nyambizi moja hadi mbili za kikosi chetu zilitekeleza kazi ya kufanya doria kwa mwaka, lakini hivi sasa idadi hiyo imeongezeka na kuwa tano hadi sita kwa mwaka, na inabidi maofisa na askari wa kikosi chetu kuishi baharini kwa siku 80 hadi 100 kila mwaka."

  Wakati huo huo, jeshi la maji la China pia linazidi kuongeza nguvu ya kufanya mazoezi katika eneo la bahari lililoko umbali mkubwa kutoka China. Kila mwaka jeshi la majini linafanya doria na usimamizi juu ya manowari na ndege za nchi za nje zaidi ya mara mia moja, na kuthibitisha udhibiti na usimamizi juu ya maeneo muhimu ya bahari.

  Kwa mujibu wa Waraka wa Mikakati ya kijeshi ya China uliochapishwa hivi karibuni na serikali ya China, jeshi la majini la China linatimiza mabadiliko kutoka kufanya ulinzi kwenye maeneo ya karibu na China kuwa kwenye maeneo yaliyoko umbali mkubwa.

  Hivi sasa jeshi la majini la China linafanya juhudi kubwa katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kimataifa ikiwemo kulinda meli kwenye eneo la bahari lililoko umbali mkubwa kutoka China, kufanya luteka ya pamoja, kutoa misaada ya uokoaji ya kimataifa, kutoa huduma za matibabu, kurejesha watu wenye uraia wa China kutoka nchi mbalimbali.

  Hivi karibuni, meli ya mizigo ya Tuvalu nambari OS 35 ilitekwa na maharamia, ambapo timu ya 25 ya kikosi cha kulinda usalama wa meli cha jeshi la China ilitoa misaada kwa nguvu mara baada ya kupokea habari hiyo, na kuwaokoa wanamaji 19. Mwongozaji wa timu hiyo Zhao Lang anasema:

  "Katika operesheni hiyo, kikosi chetu kilidhibiti mara moja meli za biashara na kuanzisha operesheni ya usakaji, ambapo tumekuwa tukitoa kipaumbele kazi ya kulinda usalama wa wanamaji na kuhakikisha mafanikio ya operesheni hiyo."

  Maendeleo ya kasi ya jeshi la majini pia yanategemea vifaa vipya. Manowari kuu ya kwanza inayoweza kubeba ndege ambayo inatengenezwa na China ilianza kutumiwa rasmi Aprili 26 mwaka huu, hali ambayo imeonesha China imedhibiti kabisa teknolojia zinazohusika za manowari ya aina hiyo na uzoefu unaohusika wa usimamizi. Mbali na hayo, vifaa vingine vya kisasa vikiwemo nyambizi zinazotumia nishati ya kinyuklia na manowari ya kufanya usakaji yenye kiwango cha zaidi ya tani elfu 10, pia vimesaidia jeshi hilo litekeleze majukumu kote duniani, na kupiga hatua kubwa katika kufikia kiwango cha juu duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako