• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Wadau wanaowapunja wasanii wa muziki Rwanda kushtakiwa

    (GMT+08:00) 2017-07-27 18:53:25

    Washikadau wanaouza kazi na kuwapunja ama kuwadhulumu wasanii wa muziki nchini Rwanda sasa watashtakiwa na kuadhibiwa na serikali ya Rwanda.

    Bodi ya maendeleo ya wasanii Rwanda imetangaza onyo hili litakaloanza kutekelezwa mwezi Agosti.

    Waziri wa biashara na viwanda Francois Kanimba amesema wamekabiliwa na changamoto nyingi kulinda haki za wasanii zikiwemo kuhakikisha wanalipwa ipasavyo baada ya kuuza kazi zao kwa washikadau.

    Wizara ya biashara tayari imeandaa mkutano na wasanii waliosajiliwa na mashirika mbali mbali ya kushughulikia kazi zao.

    Muungano wa watayarishaji wa muziki nchini Rwanda umepongeza hatua hiyo kwa kushinikiza kwamba itaimarisha sekta ya wanamuziki .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako