• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutangaza kikosi kitakachoshiriki mbio za dunia London

    (GMT+08:00) 2017-07-28 10:32:19
    Idadi kamili ya wanariadha wa Kenya watakaosafiri kwa mashindano ya dunia mjini London itajulikana leo wakati maafisa wakuu wa riadha nchini humo watakapotembelea kambi yao ya mazoezi.

    Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka kuelekea London siku ya Jumanne. Timu ya Kenya inayojumuisha wanariadha 54 , imekuwa kambi katika uwanja wa kimataifa wa Moi, Kasarani kwa wiki moja sasa.

    Hata hivyo, bingwa wa dunia kwa mbio za mita 400 Nicholas Bett, mwanariadha Alphas Kishoyian wa mbio za mita 400 na mwanariadha Michael Saruni wa mbio za mita 800, ni baadhi ya wanariadha walioko katika kambi lakini hawawezi kusafiri kwa mashindano hayo.

    Bett hatoshiriki kwa sababu ya jeraha, Kishoyian alishindwa kufikia muda wa kufuzu katika mbio za mita 400, ilihali Saruni alitemwa nje kutokana na msongamano wa wanariadha katika mbio za mita 800.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako