• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa voliboli mchangamfu kabla ya mashindano ya voliboli

    (GMT+08:00) 2017-07-28 10:32:58
    Kocha wa timu ya kitaifa ya voliboli Rwanda Jean Marie Nsengiyumva ameelezea Imani yake kuwa Rwanda itafuzu kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017, ambayo litafanyika katika mji mkuu wa Yaoundé, Cameroun kutoka Oktoba 7-14.

    Timu ya Rwanda iliwasili nchini Kenya siku ya Alhamisi kabla ya michuano ya FIVB Africa Zone V Championships ambapo itachuana na Misri, Uganda na mabingwa watetesi wa Afrika mwaka 2015 Kenya katika uwanja wa Kasarani Nairobi.

    Mashindano hayo ya siku tatu, ambayo pia yanatumika kufuzu kwa michuano ya bara, yanaanza siku ya Ijumaa (leo) na yataendelea hadi Jumapili. Timu mbili, pamoja na Kenya (bila kujali matokeo yake), yatafuzu kushiriki Kombe la Mataifa Afrika .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako