• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (22 Julai-28 Julai)

  (GMT+08:00) 2017-07-28 17:56:27

  Ethiopia kufungua kambi mpya kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

  Ethiopia itafungua kambi mpya kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan Kusini ili kukabiliana na idadi inayoongezeka ya watu wanaokimbia vita.

  Kambi hiyo mpya itakayowekwa kwenye jimbo la Benishangul Gumuz, inatarajiwa kupunguza mzigo wa kambi ya Shaerkole ambayo ni kambi kuu ya sehemu hiyo.

  Benishangul Gunuz na jimbo jingine Gambella yamewapokea wakimbizi laki 2.8 wa Sudan Kusini walioandikishwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

  Watu wapatao milioni 2 wa Sudan Kusini wamekimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe, wengi wao wamekimbilia nchi jirani za Sudan, Uganda, Ethiopia na Kenya.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako