• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la Boko Haram lashambulia kikundi cha utafutaji mafuta nchini Nigeria na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50

  (GMT+08:00) 2017-07-28 19:34:40

  Kundi la Boko Haram hivi karibuni lilishambulia kikundi cha utafutaji mafuta cha kampuni ya mafuta ya taifa ya Nigeria kwenye jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50.

  Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti kuwa shambulizi hilo lilitokea karibu na eneo la bonde la Ziwa Chad wakati kikundi hicho kilipotafuta mafuta chini ya ulinzi wa jeshi la Nigeria na makundi yenye silaha ya umma.

  Baada ya shambulizi hilo, serikali ya Nigeria ilisimamisha mara moja kazi zote za utafutaji mafuta kwenye eneo hilo. Hivi karibuni, jeshi la Nigeria liliwahi kutangaza kuwa litamkamata kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau ndani ya siku 40. Hata hivyo bado haijulikani kama shambulizi hilo linahusiana na tangazo hilo la jeshi la Nigeria au la.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako