• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya soka ya kinadada Uingereza yailaza Ufaranza

    (GMT+08:00) 2017-07-31 10:40:24

    Timu ya soka ya kinadada ya Uingereza ililaza Ufaranza kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 43 na kujikatia tiketi na kuingia kwenye nusu fainali ya Euro 2017.

    Timu hiyo maarufu kama Lionesses ilifuzu kwenye nusu fainali ambapo itachuana na wenyeji Netherlands baada ya kuisakama Les Blues ya Ufaranza ambao ilikuwa imewashinda kwa mashindano makuu matatu ya awali.

    Matokeo haya sasa yanaiweka Uingereza kama timu pekee ya daraja ya juu iliyobaki kwenye mashindano hayo baada ya Denmark kupata ushindi ambao haukutarajiwa dhidi ya Ujerumani, ambao ni washindi mara sita wa kombe hilo.

    Mshambuliaji Jonie Taylor anayechezea timu ya kinadada ya arsenal alifungia Uingereza bao lake la ushindi baada ya kufunga bao lake la tano katika mashindano hayo, na kumweka katika nafasi nzuri kushinda taji la mchezaji bora wa mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako