• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa matumizi ya uwekezaji wa nje nchini China uliendelea kuboreshwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-07-31 17:57:57

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing, ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China imeeleza hali ya biashara na nje nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Thamani ya biashara kati ya China na nchi nyingine katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imefikia yuan trilioni 13.14, na kuongezeka kwa asilimia 19.6, biashara kati ya China na nchi zilizoko kwenye "Ukanda mmoja na Njia moja" zimeongezeka kwa kasi.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema, ukubwa wa matumizi ya uwekezaji wa nje katika nusu ya kwanza ya mwaka huu umekuwa tulivu. Ushindani wa kuvutia uwekezaji kutoka nje ni mkali, na wizara ya biashara ya China imechukua hatua zilizotangazwa na Baraza la serikali la China kuhusu kufungua mlango zaidi na kutumia vizuri uwekezaji kutoka nje, pia imehimiza kuboresha mazingira ya biashara na kutuliza ukubwa wa matumizi ya uwekezaji wa nje. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China ilitumia uwekezaji kutoka nje wenye thamani ya yuan bilioni 441.5, ukipungua kwa asilimia 0.1 kuliko mwaka jana wakati kama huo, na hali ya matumizi ya uwekezaji kutoka nje ni tulivu kwa jumla.

    Mwaka jana baadhi ya kampuni za China ziliwekeza nchi za nje bila mantiki. Kuhusu suala hilo, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, idara husika za China zilifanya ukaguzi kwa makini kwa mujibu wa kanuni husika, na kuelekeza kampuni hizo kuongeza wazo wa kuepusha hatari, ili kuhimiza maendeleo safi ya uwekezaji katika nchi za nje. Takwimu zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu uwekezaji wa moja kwa moja katika nchi za nje umepungua kwa asilimia 42.9, na hali ya kuwekeza nchi za nje bila mantiki imezuiliwa kwa ufanisi.

    Katika muda uliopita, baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za nje vilikuwa na wasiwasi kuhusu mazingira ya biashara na uwekezaji nchini China, hata vilisema mazingira ya uwekezaji nchini China yamezidi kuwa mabaya. Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema, ukubwa wa matumizi ya uwekezaji kutoka nje nchini China ni tulivu, na mfumo wa matumizi ya uwekezaji wa nje pia umeboreshwa zaidi, kwa mfano, matumizi ya uwekezaji wa nje kwenye sekta ya utengenezaji wa teknolojia za juu na sekta ya huduma za teknolojia za juu yameongezeka kwa asilimia 11 na asilimia 20.

    Kwenye mkutano huo, naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa maendeleo ya Baraza la serikali la China Bw. Long Guoqiang amesisitiza kuwa, China itafanya juhudi kujenga mazingira ya biashara ya kimataifa, kisheria na kisoko, kupanua zaidi ruhusa ya kuingia kwenye soko la China kwa wafanyabiashara kutoka nje, kuhimiza ujenzi wa "Ukanda mmoja na Njia moja" na mazungumzo kuhusu maeneo ya biashara huria na makubaliano ya uwekezaji, ili kuinua kiwango cha uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako