• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yapanga kusanifu ndege zinazotumia nishati ya umeme

  (GMT+08:00) 2017-07-31 18:03:23

  Kwenye maonesho ya 13 ya safari ya ndege na safari ya anga ya juu ya kimataifa yaliyofunguliwa tarehe 18 mjini Moscow, Russia, idara nyingi za utafiti za Russia zimetoa mpango wa kusanifu ndege zinazotumia nishati ya umeme, ambao unalenga kueneza matumizi ya ndege za aina hiyo katika miaka 15 hadi 20 ijayo, kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto.

  Kituo cha utafiti cha kitaifa cha taasisi ya TsAGI ya Russia kinachoongoza utekelezaji wa mpango huo kimesema Jambo muhimu zaidi kwa usanifu wa ndege zinazotumia umeme ni kutengeneza injini za ndege zinazoaminika, na kituo hiki kitatekeleza mpango huo kwa hatua mbili. Hatua ya kwanza ni kutengeneza injini za mseto zinazotumia nishati za umeme na gesi. Hatua ya pili kutengeneza mfumo unaotumia nishati ya umeme tu, ambao utawezesha ndege inayobeba abiria 9 hadi 19 kuruka angani.

  Kituo hiki kimefanya maandalizi kwa usanifu wa ndege zinazotumia nishati ya umeme kwa miaka kumi, kimetunga mipango mingi. Hivi sasa wameanza majaribio ya kutengeneza injini kwa kipishi cha umeme kisicho na ukinzani. Lakini watafiti hawajadokeza kipishi hicho ni cha rasilimali gani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako