• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bilioni 101/- zatolewa kujenga Kidatu-Ifakara

    (GMT+08:00) 2017-07-31 19:44:44

    JUMUIYA ya kimataifa imeendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika hatua zake za kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo Umoja wa Ulaya (EU), Serikali za Uingereza na Marekani, kwa pamoja, zimetoa msaada wa Euro milioni 40.4 sawa na (Sh bilioni 101)za Tanzania.

    Fedha hizo ni kwa ajili ya kufadhili ujenzi wa barabara kuanzia Kidatu-Ifakara mkoani Morogoro, itakayojengwa kwa kiwango cha lami.

    Wizara ya Fedha na Mipango imetiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds, kandarasi ya ujenzi wa barabara hiyo, yenye urefu wa kilometa 67.

    Mradi huu utakaofungua milango ya kiuchumi kwa Watanzania kupitia Programu hiyo ya kuendeleza Kilimo.

    Ujenzi wa miundombinu una lengo la kuchochea maendeleo ya kilimo biashara kwa kuwa itasaidia kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara na wakulima.

    Barabara ya Kidatu hadi Ifakara ndiyo inayounganisha Wilaya za Kilombero na Ulanga na ni barabara kuu itokayo Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia, Malawi na nchini DRC ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako