• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yatangaza kumwekea vikwazo rais Nicolás Maduro wa Venezuela

  (GMT+08:00) 2017-08-01 10:17:41

  Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kumwekea vikwazo rais Nicolás Maduro wa Venezuela.

  Wizara ya fedha ya Marekani imesema kuwa imemtia rais Maduro kwenye orodha ya kuwekewa vikwazo ya ofisi ya udhibiti wa mali za nchi za nje. Kwa mujibu w hatua za vikwazo, mali za rais huyo nchini Marekani zitazuiwa, na wamarekani watapigwa marufuku kufanya biashara naye.

  Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin siku hiyo alisema kuwa uchaguzi wa bunge la utungaji wa katiba la Venezuela ni haramu, na mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa mjumbe wa bunge hilo huenda atawekewa vikwazo na Marekani.

  Rais Maduro mwenyewe amepinga vikwazo hivyo, lakini amesema anaona fahari kulengwa na Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako