• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AfDB kuwekeza dola bilioni 24 katika sekta ya kilimo Afrika.

    (GMT+08:00) 2017-08-01 19:20:01

    Benki ya ustawi ya Afrika AfDB itawekeza dola bilioni 24 katika sekta ya kilimo barani Afrika.

    Rais wa benki hiyo Akinwumi Adesina, amesema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi ya kimataifa ya kilimo (IITA) mjini Ibadan, nchini Nigeria.

    Adesina alisisitiza kwamba lengo la benki hiyo ni kuhakikisha Afrika ina uwezo wa kujilisha ndani ya miaka 10 na pia kutumia kikamilifu fursa zote za kilimo.

    Alisema kwa sasa Afrika inatumia dola bilioni 35 kwa mwaka kununua chakula, ilhali ina uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako