• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Makamu wa Rais wa Tanzania ataka kuongezwa juhudi za upatikanaji wa maji

    (GMT+08:00) 2017-08-01 19:22:46

    Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka wasimamizi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira kuchukua hatua zitakazowezesha kufikia lengo la Serikali la kuwapatia maji idadi kubwa ya wananchi ifikapo 2020.

    Alisema lengo la kuwa na Tanzania yenye uchumi wa kati halitatimia endapo hakutakuwa na rasilimali endelevu za maji na usafi wa mazingira.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano wa Shirika la WaterAid unaofahamika kama 'Kuweka maji safi na usafi wa mazingira' (Wash), Samia alisema watendaji na wasimamizi wa miradi hiyo wana wajibu wa kuhakikisha unafanikiwa.

    Kuhusu hali ya upatikanaji wa maji, alisema Serikali inaendelea na jitihada za kusogeza huduma hiyo kwa wananchi kwa umbali usiozidi mita 400 kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako