• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Gambia

    (GMT+08:00) 2017-08-02 09:45:20

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi jana hapa Beijing alifanya mazungumzo na mwenzake wa Gambia Bw Ousainou Darboe ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw Wang Yi amesema China imeishukuru serikali mpya ya Gambia kwa kushikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China Moja, na kufanya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kirafiki na China.

    Kwa upande wake, Bw Darboe amesema serikali ya Gambia imepongeza sera na hatua za kukuza ushirikiano na Afrika zilizotolewa na rais Xi Jinping wa China. Amesema Gambia inapenda kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji na China kwenye sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako