• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka kuhusu jeshi la India kuvuka mpaka kwa lengo la kulinda haki na usawa

    (GMT+08:00) 2017-08-02 17:47:46

    Wizara ya mambo ya nje ya China leo imetoa waraka uitwao "ukweli kuhusu kikosi cha ulinzi wa mpakani cha India kuingia ardhi ya China katika eneo la Sikkim la mpaka kati ya China na India na msimamo wa China".

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China imetoa waraka huo ili kulinda mamlaka yake ya ardhi, kutetea kanuni za kimsingi za sheria na uhusiano wa kimataifa, na kulinda haki na usawa.

    Waraka huo umesema tarehe 18 Juni kikosi cha ulinzi wa mpakani cha India kiliingia kwenye ardhi ya China, na bado kipo nchini China. Waraka huo umesema China imetoa malalamiko kwa India mara kwa mara kupitia njia ya kidiplomasia, kulaani vikali kitendo hicho, na kuitaka India kurudisha kikosi chake mara moja bila masharti yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako