• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Serikali za Benin na Rwanda kuanzisha shirika la ndege la pamoja

    (GMT+08:00) 2017-08-02 19:12:46

    Serikali za Benin na Rwanda zimesaini mkataba wa maelewano ili kuanzisha shirika la ndege la pamoja likiwa na makao yake makuu mjini Cotonou, Benin.

    Tayari shirika la ndege la RwandAir, limeanzisha safari zake nchini Benin Agosti 1.

    Benin imeipa idhini Rwanda kuendesha oparesheni zake kutoka mjini Cotonou hadi kwenye maeneo mengine.

    Ndege mpya hiyo ya pamoja itahudumu miji ya Abidjan, Brazzaville, Douala, Libreville, Bamako, Dakar na Conakry.

    Shirika la ndege la RwandAir litatuma ndege mbili za aina ya Boeing 737 mjini Cotonou na kuanza oparesheni zake katika kitovu chake kipya hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako