• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya gesi ya kupikia nchini Kenya yashuka

    (GMT+08:00) 2017-08-02 19:14:53

    Bei ya gesi ya kupikia nchini Kenya imeshuka kwa mara ya kwanza tangu mwezi Machi.

    Sasa mtungi wa kilo 13 wa gesi ni shilingi 2,073 ikilinganishwa na bei ya mwezi Juni ya shilingi 2,112.

    Hata hivyo mwaka jana bei ya bidhaa hiyo ilikuwa imeshuka hadi shilingi 2,000 baada ya serikali kuondoa ushuru.

    Kinyume na petrol, dizeli na mafuta ya taa, bei ya gesi haidhibitiwi na tume ya kudhibiti kawi (ERC).

    Kushuka kwa bei ya gesi ni afueni kubwa kwa wakaazi kwani sasa bei ya vyakula pia imeendelea kushuka kwa mwezi wa pili mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako