• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu watatu wauawa baada ya basi waliosafiria kushambuliwa mashariki mwa Kenya

  (GMT+08:00) 2017-08-03 10:10:52

  Mkuu wa kaunti ya Lamu Joseph Kanyiri amesema watu watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa jana baada ya basi la abiria walilosafiria kushambuliwa na watu wenye silaha katika kaunti hiyo karibu na mpaka wa Somalia.

  Bw. Joseph Kanyiri amesema, washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab walikuwa wamejificha kwenye msitu kando ya barabara, na dereva wa basi hilo hakutii agizo la kusindikizwa na magari ya polisi.

  Mwezi uliopita mratibu wa sehemu ya pwani ya Kenya Bw Nelson Marwa alitoa agizo kuwa ni lazima magari yote yanayosafiri katika barabara ya Lamu-Mombasa yasindikizwe na polisi, na kukaguliwa katika vituo vya ukaguzi njiani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako