• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Neymar hatimaye anagura Barcelona

  (GMT+08:00) 2017-08-03 10:31:02

  Nyota wa Brazil Neymar Junior hatimaye ataondoka Barcelona baada maombi yake ya kugura klabu hiyo kukubaliwa. Mshambuliaji huyo sasa atajiunga na miamba wa soka wa Ufaranza Paris Saint Germain kwa uamisho utakaogharimu klabu hicho pauni milioni 198 ambacho ni rekodi mpya ya fedha zilizotumika kuwahi kusajili mchezaji.

  Kwa siku za hivi karibuni Raia huyo wa Brazil hakuficha nia yake ya kuondoka Barcelona akisema angependa kutimiza ndoto yake ya kuwa mchezaji bora zaidi duniani nje ya miamba hao wa soka Uispania ambao tayari wanajivunia kuwa na washambuliaji matata Lionel Messi na Luiz Suarez.

  Hata hivyo hatua hii inajiri siku mbili baada ya kubainika kwamba Barcelona ilikuwa imeitisha uchunguzi wa FIFA ikidai PSG ilienda kinyume cha sharia kuzungumza na Neymar kwa minajili ya kumsajili bila kuhusisha klabu hiyo.

  Kando na kitita kikubwa cha usajili, Neymar atapokea mshahara mkubwa zaidi wa pauni 650,000 kila wiki bila kutozwa kodi. Nyota huyo sasa anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka mitano na klabu ya PSG baadaye leo jijini Paris.

  Neymar alihamia Barcelona kutoka klabu ya Santos nchini Brazil 2013 kwa uhamisho wa pauni milioni 46.6 na kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Uhispania 2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako