• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wauzaji vipodozi feki waendelea na biashara licha ya marufuku

    (GMT+08:00) 2017-08-03 19:19:57

    Wafanyibiashara wa vipodozi feki katika jiji la Nairobi wanaendelea kuuza bidhaa hizo kama kawaida licha ya kupigwa marufuku na shirika la ubora bidhaa .

    Wafanyibiashara hao wamesema wateja wao wameshindwa kugharamia bidhaa asili hivyo hawana budi kuwauzia ghushi kwa ajili ya kipato.

    Shirika la ubora wa bidhaa limeonya kwamba litafanya oparesheni ya awamu ya pili ,kuchunguza wanaondelea na biashara hizo kabla ya kuwati mbaroni na kuwafungulia mashataka.

    Taarifa ya mwezi huu ya shirika hilo imetoa onyo kali kwa wauzaji wakieleza hatari na madhara yake kwa watumiaji.

    Bidhaa hizo hazijasajiliwa katika bodi ya kuhkikisha ziko salama na baadhi ya wateja wamegundua uwepo wa sumu katika mchanganyiko wa baadhi ya vipodozi.

    Bidhaa maarufu zana zinazotumiwa na wanawake jijini Nairobi ni vipodozi vya uso vinavyoendelea kuwadhuru na kuchoma ngozi za wateja hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako