• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa mkoa wa Xizang wanufaika na utalii wa vijiji

    (GMT+08:00) 2017-08-04 17:38:35

     

    Kijiji cha Zhangba mkoani Xizang kiliunda shirikisho la utalii wenye umaalumu wa huko mwezi Oktoba mwaka 2010. Kuanzia wakati ule, kijiji hicho kimeshughulikia utalii unaoshirikisha chakula cha Xizang, nyimbo na ngoma, desturi ya maisha ya huko, michezo na kukaa kwenye nyumba za wakulima. Utalii umeleta faida halisi kwa kijiji hicho, na kutoa mchango mkubwa kwa juhudi za kijiji hicho kuondoa umaskini.

    Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China kwenye kijiji cha Zhangba Bw. Suolangduobujie, amesema wakati shirikisho la utalii lilipoanzishwa mwaka 2010, lilikabiliwa na matatizo mengi. Serikali ililiunga mkono na kujitangaza, na shirikisho hilo lilifanya jitihada zake. Mwaka jana shirikisho hilo lilipokea watalii zaidi ya elfu 20, na mapato kutokana na utalii yalifikia yuan milioni 4.36.

    Kijiji cha Zhangba kina familia 62. Hapo awali wanakijiji walikuwa na wasiwasi kuhusu utalii wa kijiji, familia 26 tu zilijiunga na shirikisho hilo. Lakini kutokana na maendeleo ya shirikisho hilo, watalii wengi zaidi walivutiwa na utalii wa kijiji wenye maalumu wa Xizang. Hivi sasa familia 62 zote zimejiunga na shirikisho hilo. Na mwisho wa mwaka jana familia 9 zenye matatizo kiuchumi pia ziliondokana na umaskini, na kuhamia kwenye nyumba mpya.

    Bi. Qu Ji alianza kushughulikia utalii wa Xizang mwaka 2015. Amesema kabla ya hapo familia yake iliweza kupata yuan 2,000 kwa mwaka, lakini hivi sasa kila mwezi anaweza kupata yuan 2,300, maisha yake yameboreshwa sana kwa msaada wa taifa na chama cha kikomunisti cha China.

    Katibu Suolangduobujie alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, katika kipindi cha mwanzo, shirikisho la utalii liliajiri vijana wa kijiji, baadaye liliajiri familia 9 zenye matatizo kiuchumi ili kuzisaidia kuondoa umaskini. Bw. Balu amenufaika na mradi huu wa kuwasaidia watu maskini. Bw. Balu amesema, baba ni mgonjwa na hula kitandani tu, na mtoto wake anasoma. Baada ya kuajiriwa na shirikisho la utalii, mapato yake yameongezeka, hii imepunguza shinikizo lake la maisha. Ameeleza matumaini kuwa maisha yake yanaweza kuwa nzuri zaidi kutokana na jitihada zake.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Bw. Liu kutoka mkoa wa Hubei kutalii mkoani Xizang . Amesema mazingira na hewa mkoani humo ni mazuri sana, na angependa kuishi huko kwa muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako