Katika mchujo wa kwanza Jirus Birech alimaliza katika nafasi ya tano na kufuzu kwa fainali. Birech alitumia muda wa dakika 8 sekunde 23 nukta 84.
Soufiane Elbakkali kutoka Morocco aliibuka mshindi katika mchujo huu kwa kuweka muda wa dakika 8 sekunde 22 nukta 60.
Mchujo wa pili bingwa mtetezi Ezekiel Kemboi ambaye pia ni bingwa mara nne wa dunia alimaliza katika nafasi ya nne na kufuzu kwa fainali.
Bingwa wa michezo ya Olimpiki na mshindi wa fedha katika mashindano ya dunia Conseslus Kipruto alimaliza wa kwanza katika mchujo wa tatu na kufuzu moja kwa moja katika fainali.
Aliyekuwa bingwa wa Olimpiki na vile vile bingwa wa mwaka 2017 Brimin Kipruto hakufanikiwa kufuzu kwa fainali kwani alimaliza katika nafasi ya saba katika mchujo wa tatu. Fainali ya mbio hizi itafanyika siku ya Jumanne.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |