• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kipato cha kampuni mia moja bora za mtandao wa Internet za China chazidi dola bilioni 159 za kimarekani mwaka jana

  (GMT+08:00) 2017-08-07 19:34:17

  Shirikisho la mtandao wa Internet la China na kituo cha habari cha wizara ya viwanda na habari ya China zimetoa ripoti ya pamoja, ikisema, kipato cha kampuni 100 bora za mtandao wa internent nchini humo kimezidi dola za kimarekani bilioni 159kwa mwaka jana.

  Ripoti hiyo imesema, kati ya kampuni hizo, Tencent, Alibaba na Baidu zimechukua nafasi tatu za mwanzo kwa miaka mitano mfululizo. Ripoti hiyo imesema, mwaka jana kipato cha jumla la kampuni hizo katika huduma za mtandao wa Internet kiliongezeka kwa asilimia 46.8 hadi kufikia dola bilioni 159.2 za kimarekani ikilinganishwa na mwaka 2015.

  Ripoti hiyo pia imesema, kasi ya ongezeko la kipato kinachotokana na huduma ya mtandao wa Internet kwa kampuni 72 imezidi asilimia 20, ambapo kampuni 31 kati yao zimetimiza ongezeko la kasi inayozidi asilimia 100.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako