• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jinsi buibui walivyohamia Australia kutoka Afrika Kusini katika miaka milioni 2 iliyopita?

  (GMT+08:00) 2017-08-08 09:42:20

  Watafiti wa Australia wamegundua kuwa buibui wanaoishi nchini humo huenda walihamia huko kutoka bara la Afrika katika miaka milioni 2 iliyopita.

  Kikundi cha watafiti wa Chuo Kikuu cha Adelaide cha Australia wamechambua jeni za buibui aina ya Trapdoor wanaoishi katika kisiwa cha Kangaroo, na kugundua kuwa jeni zao zina uhusiano wa karibu na wale wanaoishi nchini Afrika Kusini.

  Uchambuzi wa jeni unaonesha kuwa mababu ya pamoja ya buibui hawa kutoka Australia na Afrika Kusini wanaishi katika miaka milioni 2 iliyopita. Australia ilitengana na bara la kale la Afrika katika miaka milioni 100 iliyopita, na binadamu walifika Australia katika zama za karibuni, hivyo haiwezekani kwa buibui kuhamia Australia kupitia bara la kale wala kupelekwa nchini Australia na binadamu.

  Watafiti wanakisia kwamba mababu ya buibui hao kutoka Afrika huenda walivuka bahari ya Hindi na kufika Australia kwa kupanda miti iliyoelea baharini. Kabla ya hapo, watafiti walifikiri viumbe wengi ikiwemo buibui hawawezi kuvuka bahari ya Hindi kwa kusafiri kilomita elfu 10.

  Buibui aina ya Trapdoor wanaweza kutengeneza mtego kwa kutumia tandobui na vipande vya mimea, wanajificha ndani na kuwakamata wadudu ghafla. Watafiti wanaona kuwa mtego huo una joto na unyevu wa kudumu, ambao unawasaidia buibui kusafiri kwa umbali mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako