• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Magogo kuongoza FUFA miaka nne zaidi

  (GMT+08:00) 2017-08-08 10:19:54
  Moses Magogo ataendelea kuwa rais wa shirikisho la kandanda nchini Uganda kwa kipindi cha miaka nne ijayo baada ya kuidhinishwa katika kikao cha 93 cha kongamano la FUFA.

  Magogo ambaye amekuwa madarakani tangu 2013, alijizolea kura 69 katika ya 72 zilizopigwa katika kikao kilichomalizika bila vikwazo vyovyote.

  Kila kitu kilienda jinsi ilivyotarajiwa kwani hata ingawa Magogo alikuwa mwaniaji pekee, kongamano hilo lililofanyika Kabalega Resort Hotel lilihitaji kupiga kura kwa mujibu wa sharia za FUFA. Alihitaji jumla ya wajumbe 45 kumuidhinisha.

  Kongamano hilo lina jumla ya wajumbe 88, lakini 84 walihudhuria. Baadhi ya waliokosa kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mkurugenzi wa Proline Mujib Kasule ambaye ndoto yake ya kumwangusha madarakani Magogo iliambulia patupu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako