• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Barcelona alalamikia uhamisho wa Neymar

  (GMT+08:00) 2017-08-08 10:29:25

  Rais wa Barcelona alalamikia uhamisho wa Neymar

  Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amemkashifu Neymar kwa njia ambayo aliondoka klabu hiyo na kuingia Paris Saint Germain ya Ufaransa.

  Rais huyo alifichua kuwa Barcelona ilishuku kuwa mshambulizi huyo kutoka Brazil alitaka kukihama klabu hiyo hata baada ya kutia saini mkataba mpya mwaka wa 2016.

  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na PSG kwa kitita cha millioni 200 pauni za Uingereza ambayo ni rekodi mpya ya uamisho duniani wiki iliyopita baada ya miezi iliyojaa utata kuhusiana na uamisho huo.

  Bartomeu alisema tabia ya Neymar haikuridhisha na kwamba ni tabia ambayo klabu ya Barcelona haikutarajia kutoka mchezaji wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako