• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bomba la Mafuta kutoka Hoima hadi Tanga kuibua fursa nyingi

  (GMT+08:00) 2017-08-08 19:24:08

  Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga unaotarajiwa kuanza mwakani umeibua fursa nyingine ya kupeleka gesi ya Tanzania katika soko la Uganda.

  Hatua hiyo ilifikiwa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo unaotarajiwa kuanza mwaka kesho. Jiwe hilo la msingi liliwekwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania, John Magufuli na kushuhudiwa na viongozi kadhaa wakiwemo mawaziri kutoka Uganda na Tanzania pamoja na maelfu ya wakazi wa Tanga.

  Rais Museveni amesema nchi yake ina madini mengi ya chuma, lakini imeshindwa kuyafanya chuma halisi kutokana na kukosa makaa ya mawe au gesi, nishati ambazo ni muhimu katika kuyeyusha chuma. Rais Museveni amesema baada ya ujenzi wa bomba hilo kukamilika, ni vyema Tanzania kujenga bomba la gesi pembeni mwa bomba hilo na kuipeleka Uganda.

  Huku akihimiza ushirikiano usiishie kwenye bomba la mafuta, bali mambo mengi zaidi, Rais Museveni amesema Uganda haioni sababu ya kuendelea kutumia pesa nyingi za kigeni kuagiza chuma nje wakati ina madini hayo. Kwa upande wake, rais Magufuli amesema ombi hilo ni mwafaka na watalifanyia kazi.

  Wiki hii Mwanasheria wa Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC) Goodluck Shirima alisema bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Uganda linaweza pia kutumika kupeleka gesi katika mikoa ya Kaskazini, mikoa ya Kati na Kanda ya Ziwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako