• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa malalamiko kwa Marekani kutokana na manowari yake kuingia bahari ya visiwa vya Nansha ya China bila ruhusa

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:25:40

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema manowari ya Marekani John S. McCain iliingia kwenye bahari ya visiwa vya Nansha ya China bila ruhusa ya serikali ya China, na China imetoa malalamiko kwa Marekani.

  Bw. Geng Shuang amesema, jana manowari ya Marekani iliingia kwenye bahari ya visiwa vya Nansha ya China, na jeshi la China lilituma manowari kukagua na kuifukuzwa kwa kutoa onyo.

  Ameongeza kuwa China ina mamlaka isiyojadilika ya visiwa vya Nansha na eneo la bahari la karibu. Kitendo cha manowari ya Marekani kimekiuka sheria za China na sheria za kimataifa, kimeingilia mamlaka na kuharibu usalama wa China, na kuathiri vibaya usalama wa watu wa pande hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako