• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaendelea na kazi ya uokoaji baada ya tetemeko la ardhi mkoani Sichuan

  (GMT+08:00) 2017-08-11 16:48:36

  Hadi kufikia jana tarehe 10, tetemeko la ardhi lililotokea katika wilaya ya Jiuzhaigou mkoani Sichuan limesababisha vifo vya watu 20, na wengine 431 kujeruhiwa. Watu zaidi ya elfu 70 waliokwama kwenye eneo hilo, wamehamishwa katika sehemu salama. Hivi sasa kazi za uokoaji bado zinaendelea.

  Baada ya tetemeko la ardhi, kazi ya kuwaokoa watu imefanywa kila sehemu. Hadi kufikia saa 7 ya tarehe 10, tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 20, na wengine 431 kujeruhiwa, ambao wote wamepata matibabu. Kati ya watu 40 waliojeruhiwa vibaya, 38 wamehamishwa katika hospitali za miji ya Chengdu na Mianyang. Naibu kiongozi wa tume ya kuongoza kazi za uokoaji Bw. Qumushiha, amesema hadi sasa makazi 249 ya muda yako tayari, ambayo yamepokea watu 23,477 walioathiriwa. Bw. Qumushiha anasema,

  "Tunatumia njia mbalimbali ili kupanga maisha ya watu walioathiriwa, na kuhakikisha wanapata makazi, chakula, maji ya kunywa, nguo na vitu vinginevyo."

  Wakati huo huo, tume ya kuongoza kazi ya uokoaji pia inajitahidi kuwatafuta na kuwaokoa watu wasiojulikana walipo. Tarehe 9 tume hiyo ilipata habari kuwa watu kadhaa walikuwa wamekwama juu ya mlima Jiuzhaigou. Lakini ni vigumu kufikisha waokoaji huko kutokana na barabara kuharibiwa kabisa. Hata hivyo tume hiyo iliwatuma vikundi kadhaa vya waokoaji, huku helikopta ya jeshi ikipelekwa kuwatafuta.

  Saa 7 alasiri ya tarehe 10, helikopta hiyo iliwagundua watu waliokwama mlimani, lakini haikuweza kushuka kutokana na ukubwa wake. Hivyo helikopta nyingine mbili ndogo zilituimwana kufanikiwa kuwaokoa watu 10, isipokuwa vijana wanne bado hawajulikani walipo. Ili kuwaokoa, tume ya kuongoza kazi ya uokoaji imepanga waokoaji 15 kuendelea kuwatafuta mlimani. Bw. Qumushiha anasema,

  "Kwa mujibu wa habari tulizopata, watu hao wako kati ya sehemu ya Jianzhuhai na Xiongmaohai. Hatua tuliyoichukua ni kuwabakiza askari polisi na waokoaji 15 ili kuendelea kuwatafuta."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako