• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania yawataka wakulima kukopa kwenye benki ya wakulima

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:11:39

  Makamu wa rais wa Tanzania Bi. Samia Suluhu amewataka wakulima nchini humo kuacha unyonge na kulalamika kuhusu kutokopeshwa na taasisi za kifedha na benki. Bi Samia amesema wakulima wanatakiwa kukopa kwenye Benki ya wakulima iliyoanzishwa na serikali kwa kuwa ilianzishwa kwa ajili ya kuwainua kiuchumi.

  Akihutubia wakati wa kilele cha maonesho ya Nanenane ya kitaifa, Samia amesema serikali ilianzisha na kuweka mtaji mkubwa katika benki hiyo ili wakulima wakopeshwe. Amesema hadi kufikia sasa ni wakulima 45,000 tu ambao wameshakopeshwa shilingi bilioni 7.4.

  Kuhusu uhakika wa chakula, aliwataka wakulima kuhakikisha kwamba wanahifadhi chakula cha kuwatosha kwa mwaka mzima na kuuza ziada. Amesema Serikali haitatoa chakula kwa wilaya, ambazo zimepatwa na njaa kwa sababu ya uzembe wa watu. Amesisitiza haja ya wananchi kufanya kazi kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kuondokana na umasikini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako