• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2017-08-12 17:41:03
  Rais Xi Jinping wa China na rais Donald Trump wa Marekani leo wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu.
  Rais Xi Jinping amesema China na Marekani zinatakiwa kufuata maoni ya pamoja yaliyofikiwa kati yao mjini Hamburg, Ujerumani mwezi uliopita, kuimarisha mazungumzo na mawasiliano, kusukuma mbele ushirikiano katika sekta mbalimbali, kushughulikia kwa makini masuala yanayofuatiliwa na pande zote mbili, na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
  Rais Donald Trump amesema sasa uhusiano kati ya China na Marekani unaendelezwa vizuri na utapata maendeleo mazuri zaidi, na anatarajia kufanya ziara ya kiserikali nchini China mwaka huu.
  Marais hao wawili pia wamebadilishana maoni kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Rais Xi amesema China inapenda kuendelea kuwasiliana na Marekani kuhusu suala hilo kwenye msingi wa kuheshimiana.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako