Serikali ya Sudan imeamua kuhimiza matumizi ya dawa zilizotengenezwa nchini humo badala ya zile zilizoagizwa kutoka nje, kwa matumaini ya kustawisha sekta ya dawa ya ndani. Waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Bahar Garada amesema uamuzi huo unalenga kuhamasisha viwanda vya dawa vya ndani kwa njia ya kusitisha hatua kwa hatua uagizaji wa dawa kutoka nje. Takwimu zinaonesha kuwa Sudan inaagiza dawa zenye thamani ya dola milioni 200 za kimarekani kila mwaka, huku dawa zinazotengenezwa ndani zinachangia asilimia 40 ya mahitaji ya soko la ndani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |